SOMO: TAMBUA THAMANI YAKO KAMA KIJANA MKRISTO NDANI YA KANISA

Maandiko: 1Timotheo 4:12-16:
Mtu awaye yote asiudharau ujana wako, bali uwe kielelezo kwao waaminio, katika usemi na mwenendo, na katika upendo na imani na usafi 13 hata nitakapokuja ufanye bidii katika kusoma na kuonya na kufundisha 14 usiache kuitumia karama ile iliyomo ndani yako, uliyopewa kwa unabii na kwa kuwekewa mikono ya wazee 15 uyatafakari hayo; ukae katika hayo; ili kuendelea kwako kuwe dhahiri kwa watu wote 16 jifunze nafsi yako , na mafundisho yako. Dumu katika mambo hayo; maana kwa kufanya hivyo utajiokoa nafsi yako na wale wakusikiao pia”
“Mtu yeyote asikudharau kwa kuwa wewe ni kijana, bali uwe kielelezo kizuri kwa waaminio katika usemi, mwenendo, upendo, imani na usafi 13 fanya bidii katika kusoma maandiko hadharani, kuhubiri na kufundisha mpaka nitakapokuja 14 usiache kutumia kipawa kilichopo ndani yako ambacho ulipewa kwa neno la unabii wakati wazee walipokuwekea mikono 15 uwe na bidii katika mambo haya, jitolee kwa ajili ya mambo hayo kikamilifu, ili kila mtu aone kuendelea kwako 16 Jilinde sana nafsi yako na mafundisho yako dumu katika hayo, kwa maana kwa kufanya hivyo utajiokoa wewe mwenyewe pamoja na wale wanaokusikia

MAMBO SABA YA MSINGI YA KUKUSAIDIA KUTAMBUA THAMANI NA NAFASI YAKO KAMA KIJANA MKRISTO

1.  Ni vizuri ufahamu kwamba KABLA HAUJAZALIWA Mungu alishakujua na aliweka tayari KUSUDI,  NYAKATI, na UWEZO ndani yako maalum kwa ajili ya KANISA.{Yeremia 1:5; Zaburi 139:13,15,16;}
2. Tambua kuwa hakuna Rika lililopewa upendeleo na nafasi ya pekee kama UJANA katika Ufalme wa Mungu.{Mithali 20:29; 1Yohana 2:14; Maombolezo 3:27}

3. Licha ya uzuri mwingi ulioko kwenye UJANA, UJANA ni kipindi cha MPITO i.e. UMEPIMWA KWENYE MUDA na kwa hiyo basi UJANA HUPITA UPESI.{Mhubiri 12:1; Yohana 21:18;Matendo 17:26;Mhubiri 3:1,11}

4. Kijana ni KIUNGO MUHIMU SANA katika mwili wa Kristo yaani KANISA hivyo ni vema utambue thamani na nafasi yako katika kujenga na kuimarisha KANISA i.e. Mwili wa Kristo.{Waefeso 5:23; 1Korintho 12:27;Waefeso 4:12,16}

5. Udhaifu na Ulemavu wa KANISA LA LEO ni matokeo ya VIUNGO vingi kulala na kutofanya kazi ipasavyo, na hasa VIJANA. {Mithali 25:14;}

6. Kijana anayeweza kuleta MABADILIKO kwenye KANISA ni Yule ambaye tayari ametambua thamani na nafasi yake kama kiungo katika MWILI wa KRISTO yaani KANISA, na anatumika katika kiwango na muda husika /sahihi {Yohana 4:34}

7. Ili Kijana Mkristo atumike vizuri kwenye KANISA ni lazima ajifunze kutoka kwa Yesu. Yesu ni mfano bora wa kuigwa na kielelezo sahihi cha maisha kwa Kijana yeyote.{1Yohana 2:6; Yohana 13:15;Mathayo 12:30;Mathayo 11:29}